BIRINGI SHARKS YAVINJWA KISA GOVERNORS CUP

Mmiliki wa klabu ya Biringi Sharks Anthony Mwema anasema amelazimika kuivunjilia mbali klabu hiyo kutokana na wachezaji kukosa nidhamu na kujigawanyia pesa za zawadi za governors Cup bila kuhusisha uongozi.

Biringi sharks walikuwa mabingwa wa mashindano ya kombe la gavana katika wadi ya mji wa Malindi na walijishindia shilingi elfu hamsini katika kikosi cha wanaume lakini pia kwa kinadada ambao waliibuka mabingwa. Biringi sharks ya wanaume iliyokuwa inashiriki ligi ya kaunti sasa inatafuta wachezaji wapya baada ya tukio hilo.

”Kwa sasa tumelazimika kuivunja Biring Sharks na sasa tunaanza kutafuta wachezaji wapya baada ya hawa wengine kukaidi.” Alisema Mwema
Mwema amedokeza kuwa huenda atakalazimika kufuata sheria za nchi na kuwashtaki waluiofuja hela hizo kwani malengo ya klabu ilikuwa ni pamoja na kulipia karo wanafunzi wasiojiweza ambao ndio wengi katika kikosi cha kinadada.

”Zile pesa zingewafaa wengine ambao ni wachezaji hasa wa kike ambao pia ni wanafunzi katika shule ya upili ya barani kulipa karo. Kama hizo pesa mambo yake haitaeleweka itabidi kufuate sheria” Aliongeza Mwema