KIKOSI CHA KENYA COSAFA CHAWASILI AFRIKA KUSINI

Kikosi cha taifa cha soka cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 kimewasili rasmi huko afrika kusini kwa ajili ya mashindano ya COSAFA yatakayoanza rasmi hii leo mpaka tarehe 7 mwezi Julai.

Kulingana na benchi la kiufundi kutoka Kenya ni kuwa kikosi hicho kinalengwa kutumika kwenye mawindo ya talanta zitakazowakilisha Kenya kwenye mashindano ya Afcon 2027 ambapo Kenya itakuwa kati ya waandaaji.

Kati ya wachezaji wachanga ambao waliitwa kwenye kikosi ni Adrine Kibet , Ibrahim Wanzala na Amos Wanjala waliochini ya umri wa miaka 18.

Kenya imewekwa katika chungu B ambacho kinajumuisha Zambia, Comoros, na Zimbabwe.