Nahodha wa timu ya taifa ya soka hapa nchini Kenya Michael Olunga ni kati ya wakenya ambao wanapinga muswada wa kifedha wa mwaka 2024.
Hii ni baada ya kupachika taaarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema ‘Reject Finance Bill 2024’.
Hasira zaidi ilionyeshwa na wakenya wakidai wanalenga kufanya maandamano ya kuitimua shirikisho la soka nchini FKF kwa kukosa kuifanikisha Kenya katika siku za hivi punde, wakitishia kumtoa rais Nick Mwendwa mamlakani.
Maandamano hayo yalifanyika kote Kenya siku ya jumanne ya yalisababisha maafa na uharibifu ambao ni pamoja na watu kumi kupoteza maisha na wengine zaidi ya mia kujeruhiwa.

