Dr. AGGREY NDIO MABINGWA WA TAITA TAVETA

Kikosi cha  Soka Ya Wavulana cha Shule Ya Upili Ya Dr. Aggrey Ndio Mabingwa Kaunti Ya Taita Taveta Baada Ya Kuitandika shule ya upili ya Timbila Mabao 2-1 Kwenye Mchezo Wa Fainali Iliochezwa Dimba La Kenyatta High.

Vijana Hao Wa Mkufunzi Hamisi Masusa Sasa Wataiwakilisha Kaunti Hiyo Katika Ngazi Ya Ukanda Wa Pwani.

Wakati hayo yakijiri michezo ya hatua ya kaunti za Mombasa, Kilifi na Tana River inasalia kusitishwahadi mwezi julai kutokana na kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za michezo ya muhula huu wa pili. Kulingana na taarifa za waandaaji mashindano hayo huenda yakafanyika kuanzia tarehe 3 julai.

Mashindano ya kimkoa mwaka huu yatafanyika katika kaunti ya Tana River baada ya yale yaliyofanyika muhula uliopita kufanyika katika kaunti ya Kilifi.