Shirikisho la mpira wa wavu katika kaunti ya Kilifi linalenga kufanya mashindano ya siku mbili wikendi ijayo, mashindano yanayohusisha vilabu mbalimbali vya kaunti hii kwa leo la kuimarisha voliboli ya mashinani.
Kulingana na mwenyekiti mpya wa voliboli Kilifi Jimmy Ngala ni kuwa kwa sasa mashindano hayo ya Challenge Cup hayajapata mfadhili hivyo kulazimu, vilabu kujisimamia kwa ushirikiano na shirikisho la KVA. Pia mashindano hayo yanalenga kutumika kwenye mipango ya kuanzisha ligi ya kaunti.
” kwa sasa hatujapata mdhamini kwa hivyo vilabu vitashirikiana nashirikihso tu kuandaa mashindano haya. Tunaanza na Jumamosi na Jumapili kisha baada ya hapo tutafanya mazungumzo ya jinsi ya kuanzisha ligi yetu kama KVA” Alisema Jimmy
Mashindano hayo yanalenga kuhusisha zaidi ya timu nane huku ikiwa fursa ya kutangamana na vilabu na kujadiliana kuhusu changamoto wanazopitia mashinani. Ngala ameelezea Tama La Spoti kuwa watachukua maoni kwa viongozi wa vilabu wanaotoka sehemu mbalimbali za kaunti hiyo.

