MICHEZO YA SHULE ZA UPILI KURINDIMA MALINDI

Mashindano ya shule za upili katika hatua za eneo bunge yanaendelea katika mkoa huu wa pwani huku shule kadhaa zikitarajiwa kuandaa mashindano hayo kuanzia kesho na jumamosi.

Katika eneo bunge la Malindi, mashindano hayo yatafanyika katika shule ya upili ya lango Baya. Samuel Mulat ambaye ni katibu wa michezo ya shule za upili katika eneo bunge hilo amewarai mashabiki wajitokee kwa wingi kuhudhuria mashindano hayo.

Amedokeza kuwa kwa mara ya kwanza kutakuwa na mashindano ya raga ya kinadada kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya michezo hiyo mashinani mwa kaunti hii.

”Ningependa kusistiza mashabiki wajitokeze kwa wingi huko Lango Baya ambako mashindano hayo yatakuwa yanafanyika. Kwa mara ya kwanza kutakuwa na raga ya kinadada na kuna shule nne ambazo zimewasilisha timu zao. Kwa sasa tunaweza sema michezo Malindi imeimarika ipasavyo” Alisema Mulat