WAZAZI WASHAURIWA KUSAPOTI WANAO MICHEZONI

Wito umetolewa kwa wazazi kuwasapoti watoto wao katika michezo kama njia moja ya kuwatayarisha kwa maisha yao ya baadae.

Akizungumza na Tama la spoti kupitia njia ya simu Samuel Mulat ambaye ni katibu wa michezo ya shule za upili katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi anasema kwa ulimwengu wa sasa wanamichezo wanavuna sana kupitia michezo hivyo talanta sio za kubezwa.

Ameshauri wazazi kusaidia makuzi ya talanta za wana wao hata wakiwa nyumbani sawa na mchango anaofanya mwalimu shuleni.

”Wazazi wanafaa kuwapa sapoti wanao ili kuwafanya kukua katika michezo kwa ajili ya matayarisho kwa amaisha yao ya baadaye. Isiwe ni masomo kila wakati, kuna wakati pia watoto wanafaa kujihusisha na michezo shuleni. Kwa sasa michezo duniani inalipa vizuri. Angalia mifano ya Omanyala na Mariga ambao kwa sasa wanaishi na michezo” Alisema Mulat

Wiki jana michezo ya shule za upili iliendelea katika eneo bunge la Malindi shule kadhaa zikijitokeza kwa ajili ya mechi ya kimaeneo. Michezo katika hatua ya eneo bunge kwa mujibu wa Mulat itafanyika katika shule ya upili ya Lango Baya.