Mashindano ya shule za upili katika hatua ya kaunti za Kilifi na Tana River yameahirishwa kutoka wiki hii kuanzia siku ya alhamisi hadi tarehe 3 mwezi Julai.
Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo katika eneo bunge la Malindi ni kuwa changamoto ya kifedha imechangia kucheleweshwa kwa maandalizi hayo huku gumzo la sehemu ya kuandaa mashindano hayo ikiwa bado ni kikwazo.
Taarifa za awali zilikuwa zinasema maashindano hayo yangefanyika katika eneo bunge la Malindi kwa mara ya pili mfululizo lakini kulingana na Samuel Mulat ambaye ni katibu mkuu wa mashidano hayo ni kuwa huenda yakapelekwa katika eneo bunge la Magarini katika shule ya upili ya Marafa Boys
Kule Tana River yameahirishwa hadi tarehe 3 mwezi Julai, changamoto za kifedha pia zikitajwa kuwa kikwazo kikubwa.
Shule ya wavulana ya Ribe boys ndiyo mabingwa wa soka mwaka huu katika mashindano ya michezo eneo bunge la Rabai, baada ya kuichapa shule ya upili ya Bofu mabao 3-1 kwa njia ya matuta
Kwa upande wa akina dada shule ya upili ya wa Chang’ombe ndio mabingwa wa eneo hilo mwaka huu baada ya kuifunga timu ya Shule ya Upili ya Mikomani mabao mawili kwa moja.

