MICHEZO YA SHULE ZA UPILI MALINDI YAANDIKISHA HISTORIA

Michezo ya shule za upili katika eneo bunge la Malindi imepiga hatua kiasi cha kuandikisha historia muhula huu ya kuwa na mashindano ya raga ya wasichana ya wachezaji saba kila upande ambao watashiriki.

Kulingana na katibu wa michezo hiyo mjini Malindi kaunti ya Kilifi Samuel Mulat ambaye amezungumza na Lulu FM kupitia njia ya simu ni kuwa wasichana wa shule ya upili ya Ngala, Kakoneni, Maziwani pamoja na Barani ndio timu zilizowasilishwa msimu huu.

Mulat ameongeza kuwa walimu wa shule za upili wa Malindi wametia juhudi kufanikisha michezo shuleni.

Ametaja kuwa shule ya upili ya Barani kwenye michezo ya muhula uliopita mbayo ilihusisha sana riadha kuna mchezaji aliyenaswa na shirika la riadha nchini AK kwenda kuwakilisha Kenya mwenye michezo ya wachezaji wachanga nchini Ghana.

”Walimu Malindi saa hii wameonyesha kuwa wanapiga shuhuli nzuri sana. Kuna mchezaji anayerusha mkuki kutoka Barani saa hii alichaguliwa na AK kwenye kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20. Atasaifiri na timu ya taifa mpaka Ghana kwa mashindano ya Afrika;; Alisema Mulat.

Mashindano ya shule za upili kwa sasa yanaendelea katika kaunti za pwani mhuhula huu wa pili huku fainali za kimkoa zilitarajiwa kufanyika katika kaunti ya Tana River mwaka huu.