MICHEZO KUIMARIKA PWANI BILA MUGOKAA

Huenda michezo ikaimarika na vijana kurudi viwanjani katika mkoa huu wa Pwani iwapo utumizi wa mihadarati utazidi kupigwa marufuku katika kaunti za pwani.

Hiyo ni kulingana na Tom Lango ambaye ni mwenyekiti wa FKF katika tawi la eneo bunge la Malindi ambaye anapongeza hatua ya serikali za kaunti ya Kilifi, Mombasa, Kwale na Taita Taveta kwa kuweka sheria ngumu za kukomesha utumizi wa muguka.

Tom Lango anasema vijana wengi wameharibika na kususia michezo kisa ni uraibu wa Mugoka jambo ambalo limedororesha viwango vya soka.

”Naunga mkono serikali zetu kwa kuja na mpango wa kupiga marufuku utumizi wa mugokaa katika kaunti zetu. Wajua mara nyingi sana wachezaji huanza kutumia mugokaa saa kumi jioni ambapo huwa unashika sana. Lakini saa hii tuna imani wachezaji watatulia viwanjani. Manake wengi walikuwa wametekwa na utumizi wa dawa hizi marufuku. Tunataka soka letu liwe bila mihadarati kabisa mkoa wa Pwani.” Alisema Lango.