Timu ya kinadada ya Malindi Progressive Academy kwa sasa haishiriki ligi yoyote na wachezaji waliokuwepo takriban wote walijiondoa katika timu hiyo.
Taarifa zasema kwamba Progressive Starlets ilivunjika baada ya kushuhudiwa mgomo baridi miongoni mwa wachezaji baada ya tukio la kukosa kuheshimu ratiba muhimu ya ligi msimu uliopita.
Neema Charo ni nahodha na naibu mkufunzi kocha wa zamani wa klabu hiyo ambaye anasema kwa sasa anaendeleza shuhuli ya ukocha katika eneo la Gede baada ya kuachana na Progressive Starlets inayomilikiwa na mwakilishi wadi Rashid Odhiambo.
”Nilitoka kwa sababu kulikuwa ni kama hakueleweki. Yote hii ilianza baada ya wachezaji kuanza kugoma tulipokosa kwenda Taita kwa mechi fulani muhimu sana katika ligi yetu. Watu waliondoka ondoka nikabaki solo, pia nikajiondoa kwa sababu sikuwa na jinsi.” Alisema Neema.
Hata hivyo ukata wa kifedha umetajwa kuwa changamoto kubwa zaidiinayosibu klabu hiyo kulingana na baadhi ya viongozi waliosema na Tama La Spoti.

