Klabu ya Bumbani Stars kutoka kaunti ya Kwale licha ya kuwa huu ndio msimu wake wa kwanza katika ligi ya daraja la pili kitaifa inaendelea kuadhikisha matokeo mazuri katika ligi hiyo msimu huu.
Akizungumza na Tama La Spoti baada ya klabu hiyo kuipiga Kamtonga kutoka Taita Taveta kichapo cha mabao 2-0 wikendi ilopita,
Mwaduka bakari ambaye ni kocha mkuu wa klabu hiyo amedokeza kwamba mshikamano uliopo miongoni mwa vijana na uongozi ndio jambo ambalo linaleta mafanikio uwanjani hasa msimu huu.
Mwaduka amethibitshia Tama la Spoti kuwa klabu hiyo inaazimia kuzidi kukuza vipaji pamoja na kufikia kiwango cha kuanza kuuza wachezaji ndani na nje ya nchi. Pia ameeleza kuwa klwa sasa wapo katika nafasi nzuri ya kupanda daraja.

