OLUNGA KUNUNUA KLABU USWIDI

Nahodha wa timu ya taifa ya Harambe Stars Michael Olunga anakaribia kuinunua klabu moja huko Uswidi katika harakati zake za kutaka kuongeza umiliki wa vilabu na tasnia yake ya soka kukua zaidi.

Olunga ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Duhail ya huko Qatar anaripotiwa kutaka kuinunua AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi ya daraja la tatu ambayo kwa sasa inapitia kipindi kigumu kiuchumi.

Kwa sasa hapa Nchini Oulunga ndio mmiliki mkuu wa klabu ya MOFA inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza kitaifa, klabu ambayo Alex Mwalimu, mzawa wa kaunti ya Kilifi wadi ya Matsangoni anachezea kwa sasa kwenye msimu wake wa kwanza.

Olunga kwa sasa yupo nchini kwa ajili ya matayarisho ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa kombe la dunia 2026.

Mashindano ambayo yanaandaliwa nje ya Kenya kwani kwa sasa hakunaviwanja vya hadhi ya kuandaa mashidnao hayo kwani uwanja wa Nyayo na ule wa Kasarani vikiwa vinakarabatiwa. Mechi za kenya za nyumbani zitachezwa ugenini.