BANDARI FC KUJUA HATIMA YAO

Klabu ya Bandari FC inayoshiriki katika ligi kuu ya FKF nchini itasubiri hadi shirikishola soka FKF kupiana idhidi kwao kuutumia uwanja wa Ukunda Show Ground ulioko katika kaunti ya Kwale kwa ajili ya mechi mbili za mwisho zilizosalia kumaliza msimu huu.

Kulingana na naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Twaha Mbarak ni kuwa maafisa wa FKF walifanya ziara yao kuukagua na sasa kilichosalia ni majibu kutoka kwao kama utafikia viwango au la.

Kwa muda sasa klabu ya Bandari imekuwa ikiutumia uwanja wa Mombasa Sports Club kuandaa mechi zake za nyumbani baada ya uwanja wao halisi wa Mbaraki kufungwa kwa muda kutokana na marekebisho yanayoendelea kwa sasa.

Marekebisho yanayofanyika Mbaraki yanadhaminiwa na Kenya Ports Authority, na gharama ya takriban milioni 300M zinatarajiwa kutumika ili kuupa sura ya kimataifa uwanja huo.