McKINSTRY AIHOFIA SHABANA

Mkufunzi mkuu wa Gor Mahia amabo ni viongozi wa ligi kuu ya FKF nchini, Jonathan McKinstry ameeleza kuwa anatarajia ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wake Shabana wikendi ijayo.

McKinstry anasema Shabana ni timu inayopambana kuepuka kushuka daraja, hali halisi ambayo inamfanya kuhisi mchezo huo utakuwa mgumu kwa upande wake.

Shabana imeshinda mechi tatu na kutoka sare moja kati ya mechi nne zilizopita, na hili ndio jambo ambalo limewafanya kushika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi baada ya kutumia muda mwingi wa msimu katika eneo la kushuka daraja.