Timu ya taifa ya kinadada ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 wamepiga tizi za kutosha kwa ajili ya matayarisho ya mashindano ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia yatakayoanza rasmi wiki hii.
Junior Starlets wamekuwa kambini kwa takriban siku 10 na kulingana na kocha Charles Okere ni kuwa wako vizuri tayari kwa kupigania Kenya katika ngazi za kidunia.
Mechi ya kwanza watapiga dhidi ya Ethiopia siku ya ijumaa kabla ya kucheza mechi yao ya pili tarehe 19. Okere anasema vipusa hao wako vizuri na amewaomba wakenya kuwapa motisha na hii ni kwa manufaa ya wakenya wote kwa jumla.

