KLABU YA AC KATHAMA YAADHIBIWA

Mchezaji wa klabu ya AC Kathama klabu inayoshiriki ligi ya Fkf katika eneo bunge la Malindi mwite Bernard Tuva amefungiwa mechi mbili mfululizo kutokana na kushiriki katika mechi akijua kuwa alikuwa amepigwa kadi nyekundu katika mechi ya awali dhidi ya Bombi Fc .

Kutokana na hilo AC Kathama wamepokonywa alama zote tatu walizoshinda na kupewa Bombi kama adhabu.

Fkf inayoongozwa na mwenyekiti Tom Lango imetoa taarifa hiyo hii leo na kueleza kinaganaga sheria za mchezo kwa wachezaji kuwa mchezaji katika ligi hiyo akipigwa kadi nyekundu kulingana na shirikisho anafaa kukosa mechi mbili.

Tom Lango amewahimiza vilabu vingine kuzingatia sheria ili kuepuka adhabu kama klabu hiyo ya AC Kathama.