MAGUIRE NJE WIKI TATU

Ni rasmi sasa Harrry Maguire beki wa klabu ya Manchester United atakaa nje kwa muda wa wiki tatu kutokana na jeraha alilopata mazoezini.

Hii inamaanisha kuwa atakuwa nje kwa mechi zilizosalia msimu huu ikiwemo mechi ya fainali ya kombe la FA ambapo watakuwa wanavaana na klabu ya Manchester City katika dimba la Wembley.

Kwa sasa majeruhi Man U yameongezeka na yanamuumiza kichwa Erik  Ten Hah hasa katika eneo la ulinzi kwani Willy Kambwala, Victor Lindelof, Lisandro Martinez, Luke Shaw pamoja na Rafael Varane wote wakiwa nje.

Hii leo Man U wanacheza ugenini dhidi ya Crystal Palace mwendo wa saa nne katika mechi ya ligi kuu Uingereza.