Mkufunzi wa klabu ya Manchester United anashikilia kuwa yeye ndio mkufunzi sahihi wa kuendelea kuiongoza klabu hiyo ya Old Trafford.
Ametetea onyosho bovu la usiku wa kuamkia leo la kupigwa kichapo cha bao 4-0 dhidi ya klabu ya Crystal Palace kwenye mechi ya EPL.
Anasema kuwa majeruhi ndio yaliwaponza ikizingatiwa kuwa walinzi wake wengi wako mkekani kwa sasa.
Kwa sasa mustakabali wa Mholanzi huyo uko mashakani huku mabadiliko ya muundo yakiendelea Old Trafford tangu bilionea wa Uingereza Jim Ratcliffe kununua hisa za wachache na kuchukua udhibiti wa michezo wa klabu hiyo mapema mwaka huu.
Wikendi ijayo Jumapili Man U watakuwa wanacheza dhidi ya Arsenal katika uwanjawa Old Trafford mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya kusisimua kwa timu zote mbili ikizingatiwa msimu ndio mwanzo unaelekea kutamatika.

