Serikali ya kaunti ya Kilifi inapanga kuanzisha mashindano ya michezo mbali mbali mwaka ujao, katika mashindano ya Governors Cup yaliyoanzishwa mwaka jana chini ya gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro
Mipango hii inapanga kujumuisha riadha na michezo ya ufukweni, baada ya fainali ya soka ya governors cup kukamilika tarehe 14 mwezi ujao
Mashindano ya governors cup mwaka ujao yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi yakijumuisha michezo ya ufukweni, riadha, mpira wa wavu na soka kwa upande wa akina dada na wanaume
Mashindano ya soka ya mwaka huu ya Governors Cup yanatarajiwa kukamilika tarehe 14 mwezi wa Aprili mwaka ujao, fainali ya vijana wa kiume ikihusisha vijana wa Junju kutoka Kilifi kusini dhidi ya Sabaki kutoka eneo bunge la Magarini, upande wa akina dada mabinti wa Sokoke kutoka Gane wakivaana na wenzao kutoka Kaloleni
Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi, sherehe za kutamatisha michezo hiyo zikiwa za ufunguzi wa mashindano baina ya kaunti ya vijana wenye umri chini ya miaka 23

