Meneja wa klabu ya Gor Mahia Victor Nyaoro amesema wataimarisha kikosi chao wakiwa na matumaini ya kufuzu Kwa ligi klabu bingwa Afrika msimu ujao lakini amesisitiza kwamba usajili huo utakuwa mdogo.
Nyaoro anahisi wanahitaji kuwaamini wachezaji wao wa sasa haswa ikiwa watashinda taji la Ligi Kuu ya Kenya, na kuwazawadia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa wa CAF.
Hata hivyo anasisitiza wanamakinika zaidi Kwa ajili ya mechi 10 zilizosalia za ligi wakitumai kufikisha mataji yao hadi rekodi ya 21.
Gor kwa sasa wako kileleni, wakijivunia uongozi wa pointi saba mbele ya washindi wa pili wa msimu uliopita Tusker FC.

