Mashindano ya shule za upili yameingia katika siku yake ya pili hii leo hatua ya mkoa wa pwani katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na katibu mkuu wa mashindano hayo Mombo David ni kuwa yameonekana kuwa na nidhamu ya hali ya juu, wasichana na wavulana wakionyesha utulivu na kushiriki mashindano hayo bila taharuki yoyote.
Mashindano hayo yanahusisha michezo ya raga, riadha, mpira wa magongo, mpira wa vikapu lakini pia Handball.
Fainali zitafanyika kesho ambapo timu zitakazowakilisha mkoa mzima wa Pwani katika mashindano ya kitaifa zitabainika .
Mwaka huu mashindano ya shule za upili kitaifa zitafanyika katika mkoa wa Mashariki katika kaunti ya Machakos.

