Erling Braut Haaland amefunga mabao matano katika mechi ya hatua ya 16 dhidi ya Luton City kwenye mashindano ya kombe la FA, mechi ambayo imechezwa usiku wa kuamkia leo.
Mabao hayo yametosha kuwa fanya waajiri wake kutika hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 6-2 Luton wakiwa nyumbani kwao.
Hiyo ni Hatrick haye ya nane akiwa na uzi wa Manchester City, akiwa pia ameandikisha historia ya kuwa mchezaji wa pili katika historia ya klabu hiyo kuwahi kufunga mabao 5 katika mechi moja.
Mchezaji wa kwanza kufanya hivyo ni Sergio Kun Aguero aliyefunga mabao 5 kwenye ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Newcastle United mwaka 2015

