YOUNG BULLS YAJIANDAA KWA DABI

Meneja wa klabu ya Young Bulls Shahib Shahib klabu inayoshiriki katika ligi ya fkf daraja la kwanza anasema kwamba vijana wake wanazidi kujiimarisha kwa dabi ya wikendi hii ambapo watakuwa wanavaana na mahasimu wao kutoka mji wa Malindi United hapo kesho Jumamosi.

Amesema kuwa ana matumaini makubwa ya kusajili ushindi katika mechi hiyo ambayo yajulikana kama Mudzini Derby akizingatia kwamba kwa sasa hawana jeraha na wamekuwa wakipiga zoezi vya kutosha. Ametaja kwamba mechi hiyo sio rahisi lakini mpinzani lazima aache alama tatu.

Kiingilio katika mechi hiyo ni shilingi mia mbili za Kenya na anarai mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapiga jeki wachezaji kupitia kiingilio hicho pamoja na kuwashangilia ili kuwapa motisha.

Ametaja kuwa Young Bulls kama vilabu vingi vya pwani vinapitia changamoto za kiuchumi akihoji kuwa ada hiyo itasaidia pakubwa katika kufanikisha ratiba ya kesho katika uwanja mpya wa Young Bulls Malindi Town Secondary.