Meneja wa klabu ya Malindi United Alex Jumba amepuzia mbali semi za meneja wa klabu ya Young Bulls Shahib Shahib kuwa ataitandika Malindi United katika mechi ya Mudzini Derby itakayochezwa kesho huko Malindi Town Secondary.
Kulingana na Alex ni kuwa Malindi United imejiandaa vilivyo na kesho watasajili ushindi licha ya kuwa watacheza ugenini.
Alex anasema mashabiki wake wako vizuri kinidhamu na anatarajia itakuwa mechi ambao haitakuwa na vurugu kiupande wao tofauti na matukio ya awali. Hata hivyo ameomba mashabiki kujitokeza kwa wingi hapo kesho.
Ametoa hakikisho kuwa klabu ya Malindi United haishuki daraja msimu huu licha ya msimamo wao katika eneo la hatari katika msimamo wa jedwali. Amesema mechi kumi ambazo zimesalia anamatumaini klabu hiyo itajizatiti.
Malindi United na Young Bulls watarindimana kesho kuanzia mwendo wa saa tisa mchana huku kiingilio katika mechi hiyo kikiwa shilingi 200 ambacho ni cha kihistoria kwani hadi sasa hiyo ndio mechi inayotarajiwa kuwa na kiingilio cha juu zaidi.
Hizi hapa ndio baadhi ya kauli za mashabiki wa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na ghamu.

