FKF MALINDI YAJIPANGA

Shirikihso la soka katika eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi linajiandaa vilivyo kwa mashindano ya msimu mpya wa mwaka 2024/2025 katika ligi ya FKF ya eneo bunge hilo.

Tofauti na misimu iliyopita shirikisho limetoa taarifa kuwa kwenye suala la uhamisho wa wachezaji kutoka klabu moja hadi nyingine ni sharti taratibu zote zihusishe ofisi ya FKF tofauti na kufanya makubaliano bila kuhusisha shirikisho.

Tom Lango ambaye ni mwenyekiti wa shirikihso hilo amethibitisha kwamba kadi za wachezaji za msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Machi  zinaboreshwa vilivyo ili kuzuia wachezaji kufanya maamuzi ya kuhama kiholelela.

Ameweka wazi kuwa  klabu au mchezaji atakayekiuka sheria walizoweka za uhamisho huenda wakachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kuadhibiwa vilivyo. Huenda klabu ikapokonywa alama au mchezaji kupigwa marufuku viwanjani kwa muda.

Kwa sasa vilabu vinazidi kujiandaa kwa malipo ya usajili wa ligi hiyo huku Tama La Spoti likithibitisha kuwa vilabu vimeongezeka msimu huu tofauti na msimu uliopita kwani shirikihso linakadiria zaidi ya vilabu 30 ambavyo vitagawanywa katika maeneo mawili, Zone na Zone B.