RIGOBERT SONG AACHA KAZI

Rais wa shirikisho la soka Cameroon Samuel Etoo ametibitisha kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Cameroon Rigobert Song ameachana wadhifa huyo kwa sasa.

Etoo baada ya kikao na viongozi wengine wa shirikihso ameeleza kuwa walilazimu kutomuongeza Song mkataba kutokana na kukosa kufikia maazimio yao katika mashindano ya Afcon mwaka huu.

Ametaja kuwa wamefanya hivyo ili kuweka viwango vya juu vya soka siku za mbeleni hasa kwenye AFCON 2025 ,na sasa wanaharakati za kusaka nafasi ya kufuzu kwenye kombe la dunia 2026 na hivyo kumtakia Song maisha mema katika majukumu mengine yatakayokuja katika siku za usoni.