UCHAGUZI WA FKF WAMVUTIA SALAMBA WA YANGA

Uchaguzi mkuu wa fkf baada ya kutangazwa na waziri wa michezo wa fkf kuwa ni lazima ufanyike mwaka huu, kitaifa lakini pia mashinani umezidi kuvutia wagombea tofauti tofauti wenye manifesto zao za kuboresha michezo mashinani.

Kwa mfano katika tawi la eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, mwanaharakati wa masuala ya soka Claudius Salamba amejitokeza na kusema kwamba atakuwa kwenye debe ili kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa fkf kwa sasa Tom Lango.

Kulingana na Salamba ni kuwa katika uongozi wake vilabu mashinani vitakuwa havilipi pesa za kadi sawa na ada ya ushirika kwenye ligi kama njia moja ya kupunguza mzigo kwa vilabu ambavyo vinapitia changamoto ya ukata wa kifedha.

Vile vile Salamba ametoa hakikisho la kutia juhudi za kutafuta wadhamini watakao saidia makuzi ya talanta mashinani kupitia kudhamini sare za wachezaji, mashindano yenyewe pamoja na masuala mbalimbali.