HIZI NDIO SABABU YOUNG BULLS YAFELI

Kushuka kimchezo lakini pia kimatokeo kwa klabu ya Young Bulls kwenye ligi ya FKF katika daraja la kwanza kitaifa msimu huu ni jambo ambalo bado linazidi kuwa kitendawili kwa mashabiki wengi hadi sasa kwani tofauti na msimu janaYoung Bulls inasimama katika nafasi ya 11 kati ya timu 16 za ligi hiyo msimu huu.

Tama la Spoti kupitia mahojiano ya kipekee na Ibrahim Hemed ambaye ni msaidizi katika benchi la kiufundi ni kuwa young Bulls yenye makazi yake mjini Malindi kaunti ya Kilifi imeshuka kutokana na baadhi ya wachezaji kuweka matumaini makubwa kwa viongozi kukidhi mahitaji yao binafsi tofauti na kusimamia klabu katika mechi zake.

Amedokeza kuwa kwa ugumu wa kiuchumi klabu imekuwa ikilemea uongozi kwenye fedha za kuheshimu ratiba changamoto ambayo inatokea vilabu vingi vya mkoa huu wa pwani.

Taarifa ya mwaka jana kwamba Young Bulls ingekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu kutokana na uzinduzi wa uongozi mpya unaosimamiwa na Twahir Abdulkarim mwakilishi wadi wa Shela, Malindi kaunti ya Kilifi, Jonson Mwabati alipothibitisha kuwa angechukua wadhifa wa Uenyekiti na viongozi wengine wa serikali ya kaunti kuingia orodha ya viongozi wa Young Bulls hilo limeonekana kukosa kuzaa matunda.

Hemed amedokezea Tama la Spoti kuwa bado suala la ukata wa kifedha ni donda sugu licha ya uongozi huo mpya kudhaniwa ungeleta suluhisho.