BUMBANI FC YAPATA ALAMA KILIFI DHIDI YA YANGA

Mechi ya daraja la pili kitaifa iliyokuwa inawakutanisha vinara wa ligi Bumbani Fc kutoka kaunti ya Kwale dhidi ya Yanga FC imetamatika kwa sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Alaskan mjini Malindi kaunti ya Kilifi.

Akizungumza na Tama La Spoti baada ya mechi hiyo mkufunzi mkuu wa Bumbani Fc, Mwaduka Bakari ameeleza kuridhika na kuvuna alama moja ugenini akiwapongeza vijana wake kwa kuonyesha mchezo mzuri dimbani.

Ni mechi ambayo Bumbani wamepiga sare kwa kutoka nyuma na mabao mawili na kulazimisha sare hiyo katika kipindi cha pili.

Kwa upande Yanga FC mkufunzi Collins Omol ni kuwa kuna wachezaji wake wengi wamekosekana katika kikosi kutokana na shughuli za kikazi ikizingatiwa kuwa mechi hiyo imechezwa katikati ya wiki.

Pia ametaja uchovu ambao umewaponza sana katika kipindi cha pili mpaka mabao yakakombolewa.

Mabao hayo mawili kwa upande wa Yanga yamefungwa na Fortune Kombe na Elvis Mapinga.