Ligi ya FKF katika eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi itaanza rasmi mwishoni mwa mwezi machi mwaka huu. Hii ni baada ya makubaliano na washikadau wa ligi hiyo katika kikao kilichofanyika wikendi hii katika mji wa Malindi.
Taarifa ambazo Tama la Spoti imebaini ni kuwa basi ambalo lilinunuliwa na mheshimiwa Aisha Jumwa zama za ubunge wake katika eneo hilo linasalia bila kutumika licha ya ukarabati wake kumalizika, hii ikitokana na kukosa vibali vya kutembelea barabarani.
Kulingana na changamoto hiyo ya usafiri wa hapa na pale FKF imelazimika kuzingawanya timu za ligi hiyo kwa maeneo mawili, eneo A na B kupunguzia wachezaji gharama za usafiri.
Huku hayo yakijiri uongozi wa FKF ukiongozwa na mwenyekiti Tom Lango umetangaza rasmi kuwa kutakuwa na uchaguzi wa shirikisho unakuja na utafanyika hivi karibuni katika tarehe ambazo bado hazijathibitika.
Tom Lango ameeleza kuwa analenga kutetea wadhifa wake katika uchaguzi mkuu ujao, huku wagombea wengine wakijitokeza akiwemo Claudius Salamba ambaye ni mwanaharakati wa michezo Kilifi.

