MALINDI PROGRESSIVE ACADEMY YAJIANDAA KWA DERBY YA KILIFI

Mkufunzi wa klabu ya Malindi Progressive Nero Chishenga anasema ukosefu wa washambulizi katika kikosi chake bado ni tatizo ambalo linampa kichwa kuuma jambo linalomfanya kushindwa kushinda mechi.

Nero anasema kwamba kwa mechi za hivi punde ikiwemo ile ya wikendi ilopita dhidi ya Ziwani Youth tatizo hilo lilikuwepo licha ya wachezaji katika idara nyingine kuonyesha kiwango kizuri.

Hata hivyo anasema mabao ya mapema na yakushtukiza yalimfanya kupoteza mechi ya Ziwani Youth akihoji kwamba pia washambulizi wake walikosa nafasi nyingi za kuzalisha mabao.

Wikendi ijayo Malindi Progressive Academy inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa itakuwa na mechi ambayo ni derby ya kaunti ya kilifi inayowakutanisha na Beach Bay inayoongozwa na mkufunzi James Mkutano kutoka Magarini. Mwalimu Nero anasema mechi hiyo anajiandaa vilivyo na huenda akasajili ushindi mnono siku ya jumamosi.