Mkufunzi wa klabu ya Liverpool Jergen Klopp ameweka wazi kuwa Mohamed Salah atarejea Afcon iwapo timu yake ya taifa ya Misri itafika fainali akizingatia muda ambao mchezaji huyo anazidi kupokea matibabu.
Amesema kwamba shirikisho la soka la Misri walikubalina na Liverpool kuwa Salah akapokee matibabu Anfield ili kupata afueni ya haraka ikizingatiwa kuwa Anfield ndio kwenye matibabu bora kulingana na daktari wa mchezaji huyo.
Mohamed Salah alipata jeraha kwenye mashindano ya Afcon katika hatua za makundi na kulazimika kukaa mkekani kwa muda kabla ya kusafirishwa Uingereza kupokea matibabu.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco Wahid Regragui amefungiwa mechi nne asisimamie timu ya taifa kutokana na tukio la kuvutana na mchezaji wa timu ya taifa DR Congo.
Regragui alivutana mashati na Chancel Mbemba baada ya mchuano wa sare ya 1-1 siku ya jumapili baada ya majibizano kipindi cha pili kilipokuwa kimekamilika.
Mbali natukio hilo Regragui amepatikana na mashtaka mengine zaidi baada ya kikao cha kamati ya nidhamu ya CAF.
Hata hivyo Regragui si mkufunzi wa kwanza kupigwa marufuku katika mashindano yanayoendelea huko Ivory Coast kwani pia mkufunzi wa timu ya taiffa ya Tanzania Taifa Stars alifungiwa kutokana na matamshi yake kuhusu Morocco kuwa ilikuwa na njama ya kupanga waamuzi wao wa mechi pamoja na muda wa kucheza.
Droo ya raundi ya 16 bora ishatoka na mashindano haya yatakuwa yanarejea rasmi siku ya Jumamosi.
Nigeria vs Cameroon
Angola vs Namibia
Cape VERDE vs Mauritania
Morocco vs South Afrika
Mali vs Burkinafaso
Senegal vs Ivory Coast
Misri vs DR Congo
Guinea ya Ikweta vs Guinea Konakry
Rafiki, je wajua katika mashindano ya Afcon kwenye historia ni kipa mmoja pekee ambaye ashawahi funga bao. Ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia Kennedy Mwenee aliyefunga bao la penalty dhidi ya Nigeria mwaka 2013 mashindano yaliyoandaliwa huko Afrika Kusini.

