Mkufunzi wa klabu ya Malindi United klabu inayoshiriki katika ligi ya kitaifa ya daraja la kwanza Elly Katana amepinga kujihusisha kwa wachezaji wake katika mashindano mbalimbali ambayo sio ya ligi ya FKF.
Amesema kwamba klabu hiyo inayomilikiwa na mwakilishi wadi wa mji wa Malindi Rashid Odhiambo imeweka sheria za kuzuia wachezaji kujihusisha na mashindano kama hayo akihoji kwamba wakati mwengine ni hasara kwa klabu iwapo mchezaji atapata jeraha.
Hata hivyo amesema katika klabu hiyo ya Malindi ni kuwa wachezaji huruhusiwa kushiriki mashindano tofauti na ya ligi kipindi ambacho msimu umetamatika.
Mkufunzi huyo amesema ni sharti wachezaji wafuate sheria na wachukulie soka kama ajira tofauti na burudani pekee jambo ambalo kwa sasa limeonekana sana katika mashindano mbalimbali ambapo wachezaji wa vilabu vya ligi zinazoendelea wanashiriki. Amesema Malindi United imeweka sheria za kumtimua mchezaji iwapo atakiuka kanuni zinazopaswa kufwatwa.

