Mkufunzi wa klabu ya Mancheter United Erik Ten Hag amethibitisha kuwa Andree Onana kipa wa Cameroon atarejea rasmi katika kikosi wiki hii na huenda akawa sehemu ya timu ya the Red Devils kwenye mechi ya ligi kuu nchini uingereza Alhamisi atakapokuwa wanachuana na Wolveshampton.
Hii ni baada ya Cameroon kutimuliwa kutoka mashindano ya kombe la Afcon wikendi hii na timu ya taifa ya Nigeria katika hatua ya 16 bora.
Ten Hag amezidi kuonyesha matumaini yake kwa Onana licha ya kuwa na kiwango cha kutilia shaka. Ikumbukwe kwamba tangia Onana asajiliwe Old Trafford amekosa kucheza mechi moja pekee na ni jana dhidi ya New Port County kwenye ushindi wa mabao 4-2 katika mashindano ya kombe la FA.
Na tukiachana na Cameroon kutimuliwa katika mashindanoya Afcon kwenye hatua ya 16, wengine ambao wamewafuata nyumbani ni Misri waliokubali kushindwa kupitia mikwaju ya penalty mechi hiyo ilipotamatika sare ya bao 1-1.
Kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Guinea Konakry Guinea ya ikweta imeagana na mashindano hayo sawa na Namibia waliotolewa na Angola.
Usiku wa leo mechi mbili kubwa zitakuwa zinarindima. Cape Verde watakuwa wanatafuta kufika robo fainali watakapokuwa wanachuana na Mauritania. Mabingwa watetezi wa mashindano haya Senegal maarufu kama the lions of Teranga watakuwa wanakipiga dhidi ya wenyeji wao Ivory Coast kwendo wa saa tano.
Rafiki, je wajua kwamba timu ya mwisho kushinda Afcon wakiwa waandaaji ni Misri. Walifanya hivyo mwaka 2006 ambapo walishinda kombe hilo katika mchango wa nyumbani.
Je Ivory Coast ambao mwaka huu ndio waandaaji, wataweza? Ikizingatiwa kwamba leo wanachuana na Bingwa mtetezi Senegal?

