Shirikisho la soka hapa nchini FKF limemteuwa Mildred Cheche kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Starlets. Cheche ataisaidiwa na mkufunzi wa timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi miaka 15 Ann Aluoch.
Cheche kwa sasa ndiye mkufunzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Rising Starlets lakini pia kikosi cha Harambee Starlets na uteuzi wake unakuja kabla ya mechi ya raoundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa mashindano ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 ya FIFA mwaka 2024.
Cheche sasa anatarajiwa kusafiri na Junior Starlets hadi DR Congo kwa ajili ya mechi hiyo mwezi Februari tarehe nne mwaka huu.
Cheche mwenye elimu ya ukocha ya CAF B anachukua nafasi ya Beldine Odemba katika kikosi hicho cha Junior Starlets.

