klabu ambayo inashiriki katika ligi ya daraja la pili mwite Collins Omol amethibitisha kuwa ukosefu wa fedha ndio jambo lilopelekea klabu hiyo kukosa kuheshimu ratiba yao wikendi ilopita dhidi ya klabu ya Sparki Youth.
Kulingana na Collins ni kuwa hadi kufikia sasa klabu hiyo imekosa ufadhili jambo ambalo linazidi kuilemaza.
Mkufunzi huyo ametuma wito kwa jamii kuishikilia klabu hiyo akisema kwamba ni timu yenye uwezo mkubwa lakini inalemazwa na ukata wa kifedha.
Kwa sasa Yanga na klabu ya Mariakani ni vilabu ambavyo sasa vinasubiri uamuzi wa FKF kujua hatma yao. Yanga inatarajiwa kupiga mechi dhidi ya Teita Estate wikendi ijayo.

