Waziri wa michezo Ababu Namwamba amethibitisha kuwa serikali ya Kenya itafiatilia kwa ukaribu sana matukio yatakayofanyika katika harakati za shirikisho la soka la fkf kufanya uchaguzi mwaka huu.
Amesema kwamba ni sharti sheria zifuatwe katika uchaguzi huo, sheria za uchaguzi wa FKF zilizobuniwa na kutumika mwaka 2020.
”Serikali iko na jukumu la kufuatilia na tutafuatilia kwa ukaribu sana uchaguzi wa mwaka huu. Tunawaomba wahusika wote wafuate sheria za FKF katika uchaguzi huo” Alisema Ababu
Uchaguzi huo umevutia wagombeaji wengi akiwemo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Harambe Stars McDonald Mariga, rais wa zamani wa shirikihso hilo Sam Nyamweya, katibu mkuu wa fkf Sam Ocholla na wengineo.

