KASAYA AHAMIA 3K

Mshambuliaji matata wa klabu ya SS Assad Elmond Kasaya ameachiliwa rasmi na klabu hiyo kwenye zoezi lake la kutaka kuihamia klabu yake mpya ya 3K inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa.

Taarifa zasema kwamba klabu ya 3K inayoongozwa na mkufunzi Francis Chege imeshamsajili Kasaya baada ya kupiga tizinao kwa muda.

Kasaya sasa anatayariwa kutangazwa kama mchezaji rasmi wa 3K muda wowote kutoka sasa na kuanza rasmi kupiga soka la daraja la kwanza kitaifa wikendi ijayo dhidi ya klabu ya Kibra United.

Kasaya anaungana na nyota kama vile Alex Mwalimu walioigura SS Assad ya ligi ya kitaifa ya Super League hadi ligi ya daraja la kwanza kitaifa MOFA ya Homa Bay.

Ikumbukwe kuwa mbali na wachezaji wa Assad kuondoka mkufunzi aliyepiga kazi ya kuipandisha madaraja klabu hiyo ya Kwale Ali Mwachaunga aliondoka katika klabu hiyo baada ya kukusia mazoezi pamoja na mechi mara kadhaa mwaka jana.