Richard Masters ambaye ni Afisa mkuu Mtendaji wa ligi kuu nchini Uingereza ametoa taarifa kuwa tarehe imepangwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa madai ya ukiukaji wa sheria za kifedha , kesi inayohusu klabu ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo msimu huu.
Hata hivyo mbele ya kamati wa bunge huko Uingereza, Masters alisema hawezi kuitangaza tarehe hiyo kwa sasa.
Huku hayo yakijiri klabu ya Everton ambayo imekuwa ikiandamwa na masaibu kama hayo ilikata rufaa dhidi ya kukatwa kwa alama 10 kwa malipo ya awali, na Nottingham Forest walishtakiwa kwa kukiuka kanuni za faida na uendelevu wa ligi siku ya Jumatatu.
Manchester City klabu ambayo ilishinda Treble msimu jana ilishtakiwa kwa ukiukaji wa kanuni zaidi ya 100 mwezi Februari 2023 lakini bado hawajasikizwa kesi yao rasmi.

