TFF YAMKANA MKUFUNZI WA TIMU YA TAIFA STARS

RAIS wa Shirikisho la soka  Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa  shirikisho hilo haliungi mkono kauli ya kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars  Adel Amrouche kwamba Morocco inapanga muda na waamuzi wa michezo yao.

Amesema kauli aliyoitoa kocha huyo hivi karibuni kulishutumu Shirikisho la (CAF) na lile la nchini Morocco ni maoni yake binafsi na kivyovyote hayahusiani na TFF

Rais huyo amesistiza kuwa ratiba ya mashindano makubwa kama haya ya AFCON hupangwa kulingana na biashara za wadhamini akihoji kuwa tukio hilo pia linasaidia wachezaji wa Tanzania kuonekana katika sehemu nyingine za bara hili.

Karia amesema shirikisho la TFF litaongea na kocha huyo ili kumfanya kudhibiti kauli zake na kuepuka changamoto zingine zinazoweza kuwakuta.

Taifa Stars usiku wa leo mwendo wa saa mbili usiku itavaana na Morocco katika mchezo wa kundi “F” ambalo pia wapo DR Congo na Zambia.  Mechi ya DR Congo na Zambia itachezwa mwendo wa saa tano usiku.

Kwenye mechi za jana ni kuwa  Mali iliipiga Bafana Bafana ya Afrika kusini kichapo cha mabao 2-0 . Namibia ilishinda Tunisia kichapo cha bao 1-0 wakati Burkina Faso ikiipiga Mauritania kichapo cha bao 1-0.

Mashindano haya yanazidi kushika kazi huko Ivory Coast ambako hadi sasa yapo katika hatua ya makundi

 

.