Klabu ya Beach Bay yenye makazi yake katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi klabu inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa inalenga kusajili wachezaji watatu katika dirisha la usajiliili kukiimarisha kikosi hicho.
Mkufunzi wa klabu hiyo James Mkutano amesema kwamba Beach Bay inawinda wachezaji wawili kutoka PAG na mmoja kutoka Lubumbashy FC ili kuisaidia klabu hiyo kuandikisha matokeo bora kunako raundi ya pili ya ligi ya daraja ya pili kitaifa.
Mkutano ameahidi mashabiki wa klabu hiyo kuwa kuelekea mwisho wa msimu huu Beach Bay itazidi kuandikisha matokeo mazuri katika harakati za kutafuta nafasi ya kupanda daraja. Amesema kiwango bora kinatokana na klabu hiyo kusuluhisha changamoto kadhaa zilizokuwa zinasibu klabu hii yenye makazi yake Mjanaher
Wakati hayo yakijiri klabu ya Malindi United FC imerejesha rasmi shuhuli zake za soka katika uwanja wa Alaskan. Kwa sasa klabu hiyo ambayo zamani ilitambulika kama Malindi Progressive Academy imeanza kufanya mazoezi yao katika uwanja huo wa Alaskan.
Ikumbukwe kwamba mwaka jana Malindi United ilijiondoa Malindi na kwenda Magarini kutokana na kukosa mtakabali kamili kuhusu hatma yao ya uwanja huo ambao unamilikiwa na mwekezaji binafsi.
Hii ni baada ya mmiliki kuanza kuugawanya uwanja huo pamoja na kuonekana akifanya miradi yake binafsi katika mazingira hayo.

