MESSI AZIDI KUSHINDA TUZO ZA FIFA

Fifa usiku wa kuamkia leo imefanya tuzo za wachezaji bora wa mwaka 2023 katika jiji la London huko Uingereza. Ni tuzo ambazo zimemshuhudia Lionell Messi mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina lakini pia Inter Miami akishinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka akiwapiku washindani wake Erling Braut Haaland na Kylian Mbappe wa Ufaransa.

Timu ya taifa ya Brazil ndio waliopewa tuzo la fair play, huku kipa wa Manchester City lakini pia Brazil Ederson akishinda tuzo la kipa bora wa mwaka kwa mujibu wa FIFA.

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola ndio mshindi wa tuzo la kocha bora wa mwaka.

Baadhi ya taarifa za wachambuzi wa soka ulaya ni kuwa Messi anapigiwa upatu wa kushinda tuzo hizi baada ya kushinda kombe la dunia ambalo ndio tuzo kubwa kwa mchezaji kwa mwaka kulingana na FIFA.