LUIS SUAREZ KUUNGANA NA MESSI TENA!

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez anakaribia kusaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na klabu ya Inter Miami ya marekani ambapo sasa atakuwa anaungana na Lionel Messi mchezaji waliyesakata kabumbu pamoja enzi zao Camp Nou katika klabu ya Barcelona.

Kwa sasa taarifa zasema kwamba mazungumzo yalimalizika mwezi November na pande zote mbili kufikia makubaliani kilichosalia ni taarifa rasmi na mkataba kusainiwa rasmi.

Ni mkataba ambao utadumu kwa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuurefusha hadi mwaka 2025.

Luis Suarez amechezea vilabu kadhaa vikubwa ulimwenguni ikiwemo klabu ya Ajax ya Uholanzi kabla ya kuibukia Uingereza kukipiga katika klabu ya Liverpool na kuendeleza soka lake hata zaidi Barcelona miongoni mwa vilabu vingine.