TEITA ESTATE KUPIGA MECHI YA KWANZA DARAJA LA PILI

Klabu ya Teita Estate Fc imeratibiwa kucheza mechi yake ya kwanza katika ligi ya fkf daraja la pili kitaifa wikendi hii.

Wageni hawa sasa watachuana na klabu ya Shimanzi Fc  katika uwanja wa makande  kutoka kaunti ya Mombasa siku ya jumapili .

Teita Estate ni timu ya tatu kutoka kaunti ya taita taveta kushiriki katika ligi ya daraja la pili mbali na Jr Fc pamoja na klabu ya Kamtonga.

Teita Estate walifuzu baada ya michuano ya kuwania tikiti ya kupanda daraja baada ya kuwalaza Msato Fc kichapo cha mabao 4-0 katika fainali za michuano hiyo.