Fowadi wa klabu ya Mombasa Elite Temo Samuel ambaye kwa sasa yupo nyumbani baada ya kuachana na klabu hiyo ya Mombasa anasema analenga kujiunga na klabu ya Msabaha FC ambayo kwa sasa ipo katika kiligi ya mkoa kipindi hiki ambacho klabu hiyo inasubiri kucheza mashindano ya kufuzu kuingia ligi ya daraja la pili kitaifa.
Kulingana na Temo ni kuwa vilabu kadhaa vimekuwa vikimmezea mate lakini amekuwa akivipiga na chini ikiwemo klabu ya Malindi Progressive inayoongozwa na mkufunzi wake wa zamani Nero Chishenga.
Suala la malipo ni kati ya vigezo vinavyoumiza kichwa nyota huyu baada ya kukaushwa marupurupu yake akiwa Mombasa Elite klabu inayoshiriki ligi ya National Super League.
Temo ameambia Tama La Spoti kuwa ikiwa Msabaha itashindwa kupanda ligi ya daraja la pili kitaifa huenda akazingatia uhamisho kuelekea Malindi Progressive Academy kuungana na mkufunzi Nero Chishenga.

