MICHEZO YA KITAMADUNI KUPEWA NAFASI PIA MAGARINI

Stephen Baya ambaye ni mwakilishi wadi wa Gongoni, eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi anasema kwamba analenga kuimarisha michezo yote katika wadi yake kama njia moja ya kuinua na kuimarisha vipaji.

Amesema hayo asubui ya leo wakati akizungumza na Tama La spoti ambapo amehoji kuwa  michezo ya mipira imeangaziwa na kupewa kipaumbele sana tofauti na michezo mingine asili ya wakaazi mbalimbali wa eneo lake.

Amesema anapania kuwatambua wazee na michezo yao kama vile vigogo pamoja na talanta za nyimbo asili za kimijikenda.

”Tunataka tuanze kubambua kila michezo, sio kusema kila mara tutakuwa tunaangazia michezo ya mipira pekee lakini ni wakati sasa tuanze kuimarisha michezo hata ya kitamaduni.” Alisema Baya

Vilevile analenga kuimarisha usafiri wa vikosi vya soka vya wadi hiyo ili kusaidia wachezaji kusafiri kuheshimu ratiba katika ligi mbalimbali tofauti na sasa ambapo vijana wengi wanapitia changamoto hiyo.

”Inavunja moyo sana ukiona vijana wamejaa mitaani wanavikoba wanachangisha pesa siku ya mechi. Hilo kweli sijaliona likiwa jambo la busara na lazima tupate suluhisho” Aliongeza Baya

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *