TIMU YA ‘BANDARI STARLETS’ IPO MBIONI KUZALIWA

Uongozi wa klabu ya Bandari fc katika likizo hii umetangaza majaribio ya wachezaji wa kike katika juhudi za kuunda timu ya kinadada ya mabaharia hao kuelekea msimu ujao.

Majaribio hayo yataanza rasmi tarehe 19 mwezi huu (Agosti 2023) kuanzia majira ya asubuhi katika kaunti ya Mombasa.

Bandari Fc ni kati ya vilabu vikubwa katika taifa hili ambavyo havijakuwa na timu ya kinadada, huku ikiwa hivi punde zaidi shirikisho la soka barani Afrika Caf lilitangaza kwamba ni sharti vilabu vyote vinavyoshiriki ligi za ushirika wake kuwa na vilabu vya kinadada.

Ikumbukwe kwamba klabu ya Gor Mahia ambao waliibuka mabingwa wa ligi ya fkf msimu jana na kufuzu kushiriki mashindano ya klabu bingwa barani Afrika walilazimika kutolewa katika orodha ya vilabu vitakavyoshiriki mashindano hayo kigezo kimoja kikitajwa kuwa walikosa kuwa na timu ya kinadada mbali na mapungufu ya kukosa kulipa wachezaji kwa wakati.

Timu chache za ligi kuu ya FKF hapa nchini ikiwemo Mathare United pamoja na Ulinzi Stars ndio kati ya timu zenye wenzao kinadada.

Wapwani hao wanaoongozwa na mkufunzi Twahir Muhiddin walimaliza msimu uliopita kwa kupiga mechi 9 za mwisho bila kupoteza na hatimaye kumaliza ligi ya fkf msimu uliopita katika nafasi ya 6.