Harrison Fondo ambaye ni mwenyekiti wa zamani katika shirikisho la soka tawi la eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi ambaye sasa ni kiongozi wa vijana katika kanisa la Baptist eneo bunge la Magarini amesema kwamba kanisa hilo kwa ushirikiano na wainjilisti wa KuzaApp wanalenga kuanzisha mashindano ya michezo mbalimbali kipindi hiki cha likizo ili kuwahubiria vijana injili ya Yesu Kristo pamoja na kukuza Talanta.
Akizungumza na Tama La Spoti Fondo amesema kwamba kati ya malengo yao na washirika wake ni kuwafanya vijana ambao bado ni wanafunzi kutumia wakati wao wa likizo vyema.
”Makala ya mwaka huu yanalenga kusaidia makuzi ya talanta pamoja na kushuhulisha wachezaji mashinani. Awali tulikuwa tunafanya makongamano ya injili kwa vijana pekee lakini mara hii tunamhubiri Yesu Kristo kupitia michezo mbali mbali ikiwemo riadha, soka pamoja na michezo mingine.” Alisema Fondo.
Pamoja na hayo Fondo amesema kwamba makala ya mwaka huu yanalenga kutambua talanta za wachezaji ambazo huenda zikaangaziwa katika ngazi za juu
