OMAX FC YAJIANDAA KUPANDA DARAJA MSIMU UJAO

Klabu yenye makazi yake katika kaunti ya Mombasa Omax FC inayoongozwa na mkufunzi Juma Kalato sasa inajiandaa kuingia katika mashindano ya kutafuta tikiti ya kufuzu kuingia katika mashindano ya ligi ya daraja la kwanza kitaifa msimu ujao baada ya kuibuka mabingwa wa ligi ya FKF daraja la pili kitaifa.

Omax FC ambayo inatokea Zone A itaanza kampeni hiyo kwa kukipiga dhidi ya Dunmen Orange waliomaliza katika nafasi ya pili katika Zone B tarehe 2 mwezi September 2023 na iwapo wataibuka mabingwa basi kukipiga dhidi ya mshindi wa kati ya Ewasco FC kutoka chungu B na Simba Apparel waliomaliza nafasi ya pili nyuma ya Omax FC katika ligi ya daraja la pili kwenye eneo lao.

Fainali itachezwa tarehe 3 mwezi September mwaka huu, huku tetesi zikisema kwamba fainali huenda ikarindimwa katika uwanja mmoja katika kaunti ya Mombasa.